Submit your work, meet writers and drop the ads. Become a member
waiting for Jina;
can't write poems
till he comes back
comebacksoon.  http://www.youtube.com/watch?v=vqc2uOunPdA
andrew juma Jan 2016
Hapa ndipo umenifikisha
Umalenga na ujopo
Wa kiingereza tulimudu
lakini kiswahili kitamu
**** la mama litamu
Hata liwe la mbwa

Kimombo kilaini majineno
Kama mayai ya johari
Kuangaza mitima halaiki
Namshukuru Rabuka
Kwa talanta ya kuandika

Tukaumba kwa maneno
Waumbaji nikawaunga
Kama yeye Mungu,
Nguvu za maneno kat'tunukia

Uwezo wa karana hii
Kuwateka akilizo
Nyika na mito kuwavusha
Hadi sayari za ndoto zao
Uswahilini narudi mie
Kitamu kwelikweli

Nashukuru Maulana
Kipaji nilipata
Naye ataniauni
Dau langu lifike kilindini
Nitue kileleni

Niangaze kama Zuhura
Hapa ndipo nimefika
Umalenga na ujopo
N'taukumbatia milele
Kwa Kiswahili na kimombo

Mitima zao kusisimua.
Standby for translation...
andrew juma Jan 2016
Chini ya mnazi bandarini
Kumbukumbu ndizo zilizobakia tu
Kunizinguka akilini
Huba lako kulikosa
Yaumiza moyoni

Upepo  kutoka baharini
Tulipoketi ukininong'onezea
Sikioni kwamba ni mimi tu
Kwamba utanipenda
Tukichora zetu mchangani
Aaah, nyakati za raha hizo!

Ukaniliwaza mtima
Tukapanga mipango ya milele
Nabakia kutafuna utamu
Wa kumbukumbu tu
Chini ya mnazi bandarini
Nikilemewa maradhi ya moyo

Filamu ya huba letu akilini
Tukicheza ufukoni
Penzi ndio madini ninayokosa mwilini
Kama kosa ni langu najuta
Usinkwepe rejea nakwita

Nitakuenzi nikutunze almasi
Tulitwae tunda la penzi nawe
Tulichovye buyu la asali
Wengine waone kijicho

Tupendane tena
Chini ya mnazi bandarini
Come back sweet love!
Translation's up next...
JB Sep 2018
oldest word in the english langu
age with me and we can have a f
east to where the sun rises and w
estuaraies full of vibrant life with
thering vines where grapes once g
rue the day!

— The End —